• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mchezaji wa Juventus akutwa na Virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-12 17:18:37

    Klabu ya Juventus imetangaza kuwa mchezaji wake, Daniele Rugani amekutwa na maambukizi ya virusi vya corona. Klabu hiyo ya ligi ya Serie A imesema kwamba imechukua hatua zote za kumtenga mchezaji huyo zinazohitajika kisheria ikiwemo kuwashirikisha wale ambao waligusana naye. Klabu hiyo imeongezea kwamba Rugani mwenye umri wa miaka 25 kufikia sasa hajaonesha dalili za ugonjwa huo. Italia imerekodi visa 12,000 vya maambukizi na vifo 827 kutokana na virusi hivyo. Wakati huohuo, nyota wa Hannover 96, Timo Hubers naye amekuwa mchezaji wa kwanza wa kulipwa kukutwa na virusi vya korona nchini Ujerumani. Beki huyo yuko chini ya uangalizi katika nyumba za wagonjwa, na wafanyakazi wengine waliowasiliana naye kwa karibu watapimwa na kufuatiliwa afya zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako