• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kocha awataka wachezaji wapya kikosini wapiganie nafasi katika timu

    (GMT+08:00) 2020-03-12 17:18:56

    Kocha Mkuu wa Gor Mahia Steven Polack amewataka wachezaji wapya ambao walisajiliwa na timu hiyo wapiganie nafasi yao katika timu, huku mbio za kuwania taji la Ligi Kuu (KPL) zikiwa kwenye mkondo wa lala salama. K'Ogalo ambao ni mabingwa watetezi wapo kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa na alama 54, saba mbele ya Kakamega Homeboyz ambayo bado ina mechi moja zaidi huku zikiwa zimesalia mechi tisa kabla ya msimu wa 2019/20 kumalizika. Baadhi ya wachezaji waliosajiliwa na Gor mwezi Januari ni raia wa Uganda Juma Balinya, Mghana Jackson Owusu, Clinton Okoth na Nicholas Omondi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako