• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ECW yakadiria kuwa watoto wa kike milioni 39 katika nchi zilizoathiriwa na mapigano ya silaha wanakosa elimu

    (GMT+08:00) 2020-03-12 18:38:42

    Inakadiriwa kuwa watoto wa kike milioni 39 katika nchi zilizoathiriwa na mapigano ya kutumia silaha, waliolazimishwa kukimbia makazi yao ama majanga ya asili wanakosa nafasi ya kupata elimu bora.

    Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Haiwezi Kusubiri (ECW) amesema, watoto hao wanawakilisha kizazi kipya wanazuiwa kupata ujuzi wanaohitaji kukabiliana na migogoro hiyo, kujenga upya maisha yao na kutoa mchango katika ukarabati mpya wa jamii yao.

    Ametolea mfano nchini Sudan, ambapo asilimia 72 ya watoto wa kike wenye umri wa kwenda shule ya msingi hawapati fursa hiyo, huku katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya, asilimia 38 pekee ya wanafunzi wanaohudhuria shule ya msingi ni wasichana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako