Waziri wa Utalii na Wanyamapori Najib Balala alisema sehemu ya fedha hizo zitatumika kurudisha imani na kuhakikisha kuwa Kenya inabaki kuwa eneo linalopendwa kwa usafiri duniani.
Fedha nyingine zitatumika katika mkakati wa ufufuaji wa masoko makuu ya watalii wanaokuja Kenya.
Waziri Balala aliyasema hayo jana wakati akihutubia wadau wa sekta ya utalii jijini Nairobi.
Mkutano huo uliandaliwa na Wizara ya Utalii kujadili utayari wa serikali ya Kenya kuhusiana na sekta hiyo kufuatia janga la kimataifa la COVID-19.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |