• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bajeti ya Tanzania yaongezeka kwa Sh.trilioni 1.7

    (GMT+08:00) 2020-03-12 18:44:17
    Serikali inatarajia kukusanya na kutumia Sh. trilioni 34.88 katika mwaka ujao wa fedha, huku Sh. trilioni 21.98 zikitengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida zikiwamo gharama za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

    Bajeti hiyo ya tano chini ya uongozi wa Rais John Magufuli, imeongezeka kwa Sh. trilioni 1.7 kutoka Sh. trilioni 33.1 zilizotengwa kwa mwaka huu wa fedha.

    Imeelezwa na serikali kuwa bajeti hiyo imezingatia mahitaji halisi ya ugharamiaji miradi mikubwa ya kimkakati, ulipaji mishahara, deni la serikali na vipaumbele vingine vya taifa.

    Akiwasilisha kwa wabunge jijini Dodoma jana Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa, Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/21, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, alisema serikali imejipanga kikamilifu katika maandalizi ya uchaguzi mkuu ikijumuisha mahitaji ya kibajeti ili kuufanikisha.

    Mwezi Oktoba mwaka huu, Tanzania itafanya Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako