• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • DR Congo kuchelewesha ujenzi wa daraja la kwenda Brazzaville

    (GMT+08:00) 2020-03-12 18:44:54

    Daraja la kiungo lilopangwa kujengwa kati ya Kinshasa na Brazaville huenda likawa sio kipaumbele tena kwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

    Haya ni kwa mujibu wa maafisa wanaoshughulika na mradi huo.

    Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mipango wa DRC,Bi Elysée Munembwe, amesema kuwa mradi huo utacheleweshwa huku serikali ikishughulika na mambo mengine muhimu zaidi.

    Hayo yamejiri baada ya upembuzi yakinifu kukamilika na ujenzi katika daraja hilo lenye urefu wa mita 1,757 kupangwa kuanza mwezi Agosti.

    Mradi huo ungetekelezwa na ufadhili kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambayo makubaliano na kanuni yamekwisha kufikiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako