Kaimu mkurugenzi mkuu wa Kamati ya biashara ya hisa ya Nigeria Mary Uduk amesema, kushuka kwa bei ya mafuta wakati mlipuko wa virusi vya korona umetokea duniani kutaathiri vibaya soko la mitaji la nchi hiyo.
Ameongeza kuwa, bajeti ya taifa ya mwaka 2020 ya Nigeria tayari inatishiwa kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta, lakini juhudi za kina zinatakiwa ili kukabiliana na suala hilo ambalo linaathiri ni alama kwa ajili ya mafuta ghafi.
Bi. Uduk amesema, tayari serikali ya Nigeria imekutana na Benki Kuu ya nchi hiyo ili kutafuta njia za kukabiliana na hali hiyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |