• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama la UN larefusha muda wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2020-03-13 09:29:08

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kurefusha muda wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS hadi tarehe 15 mwezi Machi mwakani.

    Azimio nambari 2514 limeamua kudumisha kazi ya tume hiyo yenye askari wasiozidi elfu 17 na polisi wasiozidi 2,101. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia limesema litafanya marekebisho kwa tume ya UNMISS kulingana na hali ya usalama huko Sudan Kusini, pia limezitaka pande zote husika zisimamishe mapambano nchini humo na kuanzisha mazungumzo ya kisiasa.

    Barala la Usalama la Umoja wa Mataifa linataka serikali ya Sudan Kusini iache kuizuia tume ya UNMISS kufanya operesheni, na kuacha kuwazuia wadau wa kibinadamu kuwasaidia raia, ili kuhimiza kusimamisha vita na kuhimiza kazi ya usimamizi wa usalama nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako