• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China afanya mazungumzo kwa njia ya simu na katibu mkuu wa UM

    (GMT+08:00) 2020-03-13 10:06:15

    Rais Xi Jinping wa China jana usiku alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. António Guterres.

    Katika mazungumzo yao rais Xi amesema baada ya juhudi kubwa, China imepata mwelekeo mzuri katika kuzuia na kudhibiti maambukizi ya nimonia ya COVID-19 inayosababishwa na virusi vipya vya korona, huku mchakato wa kurejeshwa kwa utaratibu wa kawaida wa uzalishaji mali na maisha ukiharakishwa. Amesema katika kipindi kijacho China itaimarisha kinga na udhibiti wa maambukizi ya ugonjwa huo, na kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii. Pia amesisitiza kuwa, maambukizi ya ugonjwa huo yameenea katika nchi nyingi duniani, jumuiya ya kimataifa inatakiwa kufanya ushirikiano wa kimataifa katika kuzuia na kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo kwa pamoja.

    Kwa upande wake Bw. Guterres amesema Umoja wa Mataifa unaishukuru China kwa kutoa misaada kwa nchi zinazokabiliwa na maambukzi ya ugonjwa huo, na kwamba Umoja wa Mataifa unatarajia kukuza ushirikiano na China katika sekta mbalimbali na kutarajia kuwa China itachukua nafasi ya uongozi kwenye mambo ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako