• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ghana na Gabon zathibitisha kutokea maambukizi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-13 10:06:31

    Wizara ya Afya ya Ghana imethibitisha kuwa watu wawili wa wameambukizwa virusi vya COVID-19 nchini humo.

    Waziri wa mawasiliano wa Gabon Bw. Edgard Miyakou naye ametangaza kuwa mtu mmoja amethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo nchini humo. Mtu huyo ni raia wa Gabon aliyewasili nchini humo kutoka Ufaransa tarehe 8 Machi.

    Nchi mbalimbali za Afrika zimechukua hatua kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo. Algeria na Morocco zimekubaliana kusimamisha safari za ndege kati yao. Serikali ya Sudan imetangaza uamuzi wa kupiga marufuku raia wa nchi zinazoathiriwa na maambukizi ya ugonjwa huo kuingia nchini Sudan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako