Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amependekeza mawaziri 35 katika baraza la mawaziri la serikali ya mpito baada ya uundaji wa baraza hilo kucheleweshwa kutokana na migongano na kundi kuu la upinzani la SPLM-IO. Kwa mujibu wa makubaliano ya amani yaliyofikiwa mwaka 2018 nchini Ethiopia, upande wa serikali umependekeza 20 kati ya nafasi 35 za ngazi ya mawaziri, kundi la SPLM-IM limepata nafasi 9, huku vyama vingine vikipata nafasi zilizobaki.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |