• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KIKAPU: Ligi ya kikapu (RBA) kuendelea tena leo

    (GMT+08:00) 2020-03-13 12:12:01

    Ligi ya Mpira wa kikapu mkoa wa Dar es Salaam (RBA) inaendelea leo kwa timu za maafande kupambana kusaka ushindi katika mzunguko wa tatu. JKT inayokamata nafasi ya pili kwenye msimamo itaikaribisha Polisi ambayo imetoka kujeruhiwa katika mzunguko uliopita dhidi ya Chui kwa pointi 58-42. Mechi hiyo ya saa 10 jioni itachezwa kwenye uwanja wa ndani wa Taifa ikifuatiwa na ile ya Mgulani JKT dhidi ya ABC saa 12 jioni uwanjani hapo. JKT Mgulani itashuka uwanjani ikiwa haijaonja ladha ya ushindi katika mechi zake mbili ilizokwishacheza msimu huu wa RBA huku ABC inayoongoza kwenye msimamo kama itashinda mchezo huo, itakuwa ni mechi yake ya tatu kushinda mfululizo. Keshokutwa Jumamosi, vigogo Savio wataikaribisha timu yenye historia ya kushuka daraja mara kadhaa ya Outsider wakati Don Bosco Youngstar wakiumana na Chui. Oilers yenyewe itakuwa na kibarua dhidi ya Magnet wakati timu ya Tanzania ya vijana chini ya miaka 18 ikiikabili Mabibo Bullets na DTB ikiumana na Ukonga Kings. Bingwa mtetezi timu ya Vijana ambayo ilianza vibaya mechi yake ya ufunguzi, itacheza na Pazi. Jumapili, Don Bosco Youngstars itakuwa na kibarua dhidi ya Savio, Ukonga Kings itaikabili JKT Mgulani, Mabibo Bullet itacheza na Chui, Kurasini Heat itaikaribisha Polisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako