• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kocha Azam FC arambwa faini kwa kukataa kuongea na wanahabari

    (GMT+08:00) 2020-03-13 12:13:17

    Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imemtoza faini ya Sh. 500,000 kocha Mkuu wa Azam FC, Mromania Aristica Cioaba kwa kosa la kugoma kuzungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya mechi dhidi ya Simba SC Machi 4, mwaka huu Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Cioaba aliyeonekana kutopendezewa na maamuzi ya marefa katika mchezo huo ambao timu yake ilichapwa 3-2 na Simba SC, ameadhibiwa kwa kuzingatia Kanuni namba 41 (12) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha. Simba nayo imepewa onyo kali baada ya kuchelewa na kufika Saa 12:45 badala ya saa 12:00 katika mchezo huo na onyo lao kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo.

    Kocha Msaidizi wa Polisi Tanzania, Ally Mtuli anapelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kumshambulia mwamuzi msaidizi Neema Mwambashi na kumtolea matusi ya nguoni kwenye mechi dhidi ya Mwadui FC walioshinda 2-1 Machi 4 pia Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako