• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti feki ya virusi vya COVID-19 ya gazeti la Daily Nation Kenya yalaaniwa  

    (GMT+08:00) 2020-03-13 16:43:00

    Gazeti la Daily Nation la Kenya jana lilitoa ripoti kuhusu mwanafunzi wa Kenya anayesoma katika Chuo Kikuu cha Chang'an China alivyojiweka karantini kwa siku 14 baada ya kurudi Kenya. Lakini kicha cha ripoti hiyo kinasomeka "Coronavirus: Kenyan student happy to be home from China 'hell'", tafsiri ya haraka ni kwamba mwanafunzi wa Kenya anafurahi kurudi nyumbani nyumbani kutoka jehanamu ya China. Jambo la ajabu ni kwamba, kwenye ripoti hiyo mwanafunzi huyu hajawahi kusema kuwa China ni jehanamu.

    Mwandishi wa habari aliwasiliana na mwanafunzi huyo aitwaye Bernard Muthuri. Mwanafunzi huyu alisema alipoona ripoti hiyo alikasirika sana, alimwuliza mhariri wa gazeti hiyo: "Lini niliwahi kusema China ni jehanamu? Kwa nini ulitumia kichwa cha habari cha namna hiyo? Hayo ni maoni yangu, niliandika tu maisha yangu ya karantini kwenye ukurusa wangu wa Twitter, na kusisitiza umuhimu wa kujiweka kwenye karantini."

    Gazeti hilo lilirekebisha kichwa cha habari kwenye tovuti yake, lakini nakala ya magazeti yaliyochapichwa hayawezi kufanyiwa marekebisho, na kuichafua sana China.

    Basi maisha ya Bw. Muthuri yalikuwaje nchini China? Bw. Muthuri amesema maisha yake nchini China yalikuwa kama kawaida, chuo kikuu kiliwapatia wanafunzi vitu vinavyohitajika ikiwemo chakula na mask, na kuwataka wasitoke nje kama hakuna ulazima. Alirudi Kenya ili kuondoa wasiwasi kwa familia yake. Jambo la kufurahisha ni kuwa chuo kikuu kinatoa mafunzo kupitia mtandao wa Internet, hivyo anaweza kuendelea na masomo akiwa nchini Kenya.

    Hii si mara ya kwanza kwa gazeti hili kuchafua sifa ya China. Awali, gazeti hili lililitumia maneno ya China Virus (Virusi vya China) na kupingwa na Wachina wanaoishi nchini Kenya. Sababu ya Shirika la Afya Duniani kuvipa virusi hivi jina la COVID-19 ni kutohusisha virusi na nchi na sehemu yoyote. Kazi muhimu ya vyombo vya habari ni kuzuia ukosefu wa uelewa kwa sayansi, kuzuia uonevu kwa ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako