• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Betway Cup raundi ya 16 kuchezwa wikendi nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2020-03-13 16:55:41

    Ligi Kuu ya Kenya (KPL) itapumzika wikendi hii kupisha michuano Betway Cup raundi ya 16 Bora itakayoshuhudiwa katika viwanja mbali mbali nchini humo. Katika michuano hiyo ya muondoano, kesho Jumamosi kuanzia saa saba itakuwa zamu ya Wazito FC na Kenya Commercial Bank (KCB) katika uwanja wa Afraha Nakuru, kabla ya Gor Mahia kuingia uwanjani humo baadaye kucheza na Posta Rangers. Mechi nyingine zitakazochezwa kesho ni ile ya Bandari ambao watakuwa wenyeji wa Sofapaka kuanzia saa kumi katika uwanja wa Mbaraki Sports Club, Mombasa. Jumapili, Ulinzi Stars watakuwa wenyeji wa Migori Youth ugani Afraha Nakuru kuanzia saa saba, kabla ya AFC Leopards kujibwaga uwanjani humo kukabiliana na Ushuru FC kuanzia saa tisa unusu. Timu ya Fortune Sacco inayoshiriki Supa Ligi ya Kenya (NSL) itakuwa nyumbani uwanjani Kianyaga kesho Jumamosi kucheza na Bidco United kuanzia saa tisa. Mjini Kisumu siku ya Jumapili, mashabiki watamiminika Moi Stadium kushuhudia pambano kati ya wenyeji Kisumu All Stars na Keroka Technical University, huku Kariobangi Sharks wakipepetana na FC Talanta ugani MISC, Kasarani. Bingwa wa Betway Cup atapokea Sh2 milioni mbali na tiketi ya kuwakilisha Kenya katika mashindano ya CAF Confederations Cup, msimu ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako