• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaunga mkono kampuni nchini humo kuchangia udhibiti wa COVID-19 duniani

    (GMT+08:00) 2020-03-13 18:00:55

    Mkuu wa idara ya biashara ya nje iliyo chini ya wizara ya biashara ya China Bw. Li Xingqian amesema, hivi sasa uzalishaji umerejeshwa katika kampuni nyingi zaidi za uuzaji bidhaa nje ya China. Wizara hiyo itaunga mkono kampuni hizo kuharakisha kufufua uzalishaji, na kutoa mchango kwa ajili ya udhibiti wa maambukizi ya COVID-19 kote duniani.

    Bw. Li Xingqian amesema, kutokana na maambukizi ya COVID-19 pamoja na mapumziko ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, wakati wa kuanza tena uzalishaji wa kampuni hizo umechelewa kuliko mwaka uliopita, hivyo biashara na nje katika miezi mwili ya kwanza ya mwaka huu, hususan uuzaji bidhaa kwa nje umeshuka kwa kiasi. Lakini amesema katika kipindi hiki, bidhaa zenye sifa bora, teknolojia ya juu na thamani ya ongezeko ya juu zimeuzwa kwa wingi zaidi, na bidhaa kuu zinazoagizwa kutoka nje zinaongezeka.

    "Ili kupunguza athari ya maambukizi ya COVID-19, wizara ya biashara ya China pamoja na idara mbalimbali husika zimetoa sera nyingi za kutuliza biashara ya nje, kuunga mkono kampuni za biashara ya nje kufufua uzalishaji, kufanya juhudi zote kulinda soko na kuhakikisha oda. Hivi sasa, ufanisi wa sera hizo umeonekana, kampuni za sehemu mbalimbali zimeharakisha mchakato wa kufufua uzalishaji, na uwezo wa kutekeleza mikataba umeongezeka. "

    Mkutano wa Baraza la Serikali la China uliofanyika hivi karibuni pia umetunga mpango mpya kuhusu kutuliza biashara ya nje na uwekezaji kutoka nje, ikiwemo kuelekeza mashirika ya kifedha kuongeza utoaji wa mikopo kwa biashara za nje, kufanya maandalizi ya maonyesho ya bidhaa ya Guangzhou ya majira ya spring, na kuhimiza kwa nguvu ushirikiano wa biashara.

    Bw. Li Xingqian amefahamisha kuwa, wizara ya biashara ya China inakamilisha zaidi mfumo wa kazi ya kutuliza biashara ya nje, na kutumia umuhimu wa soko katika kugawa rasilimali.

    "Idara za serikali zimechukua hatua mbalimbali za kurahisisha mchakato wa kutoa idhini uagizaji bidhaa kutoka nje, kupunguza muda wa kutoa idhini. Tunajitahidi kutoa huduma za utoaji wa habari za mahitaji na uzalishaji, kuimarisha maingiliano na nje, kufanya umuhimu wake wa mawasiliano na kuzisaidia kampuni hizo kukabiliana na athari ya COVID-19. Kufanya kazi ya aina mpya za biashara ya nje, kukusanya habari za soko la kimataifa, kupanua chanzo cha bidhaa, kutumia ghala za kampuni ya biashara ya mtandao ya kuvuka mpaka katika nchi za nje na usafiri wa kimataifa, pia kuinua kiwango cha kuagiza na kusambaza bidhaa. "

    Bw. Li pia amesema China ina uwezo mkubwa wa biashara ya nje, na kampuni za China zina uwezo mkubwa wa uvumbuzi na kupanua soko. Amesema wizara ya biashara ya China itaendelea kuunga mkono kampuni zake kutoa mask na vifaa vingine vya matibabu kwa nchi za nje, na kuchangia inavyowezekana kwa ajili ya udhibiti wa maambukizi hayo kwa dunia nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako