• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalam na vifaa kutoka China vyawasili Italia wakati nchi hiyo ikijitahidi kudhibiti COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-13 18:28:11

    Timu ya madaktari wataalam kutoka China pamoja na tani 31 za vifaa vya matibabu imewasili Italia jana jioni wakati nchi hiyo ikijitahidi kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona (COVID-19) ambayo mpaka sasa yamesababisha vifo vya watu zaidi 1,000.

    Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu Bw. Francesco Rocca amesema Italia inaipongeza China katika mapambano yake dhidi ya virusi vya korona, na inaishukuru China kwa kutoa msaada na kuiunga mkono katika wakati huu mgumu.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia Luigi Di Maio pia ameishukuru China kwa kupeleka timu ya madaktari na kutoa vifaa vya matibabu ya dharura.

    Akizungumza katika uwanja wa ndege wakati wa kupokea timu ya madaktari na vifaa, balozi wa China nchini Italia Li Junhua amesema, virusi havijali mpaka, na nchi zinapaswa kuunganisha juhudi zao ili kudhibiti virusi hivyo.

    Italia imeathirika zaidi na maambukizi ya virusi vya korona baada ya China, na mpaka sasa, idadi ya kesi za maambukizi imefikia 12,839.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako