Mchumi wa Kilimo kwenye jumuiya hiyo Fahari Marwa, amesema pendekezo la ufadhili wa Muswada huo limewasilishwa kwa USAid na kuongeza kuwa ikiwa litapitishwa hatua hiyo itasaidia kupunguza hatari ya kukosekana kwa chakula na ugonjwa wa saratani inayotokana na sumu kwenye nafaka.
Marwa ameyasema hayo wakati wa mkutano wa utekelezaji wa mkakati wa kikanda wa EAC na mpango wa utekelezaji kuhusu udhibiti wa kinga ya aflatoxin jijini Nairobi.
Mkutano huo, ambao tayari umefanyika katika nchi zingine wanachama, unakusudia kujadili hatua za kupunguza athari ambazo husababishwa na sumu kwenye nafaka.
Mwaka wa 2017 baraza la mawaziri la EAC lilikubaliana nchi zote wanachama zitenge pesa ambazo zitatumika mahsusi katika kutekeleza mkakati wa kukabili aflatoxin.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |