• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Emirates yasitisha safari zake Uganda

    (GMT+08:00) 2020-03-13 19:50:46
    Shirika la ndege la Emirates limesitisha safari zake kadhaa kutoka Dubai hadi Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe nchini Uganda, ikitoa sababu za kiutendaji.

    Emirates lilitoa taarifa ikionyesha kwamba ni ndege za Jumatatu na Jumatano tu zitakazoathrika kuanzia Machi 18 hadi Aprili 29.

    Meneja mauzo wa Emirates nchini Uganda Bi Sarina Carrasco, amethibitisha kufutwa kwa safari hizo lakini hakutoa maelezo zaidi.

    Alisema taarifa ya kufutwa kwa safari hizo ilitolewa na ofisi kuu ya Emirates na kwamba taarifa ya kina itatolewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako