• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kwa nini idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa COVID-19 barani Afrika ni chache

    (GMT+08:00) 2020-03-14 18:48:21

    Hadi sasa, jumla ya nchi 17 za Afrika zimeripoti maambukizi ya ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19, na idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi hivyo ni zaidi ya 150. Ikilinganishwa na nchi za mabara ya Asia na Ulaya, idadi hiyo ni chache sana.

    Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kukinga Magonjwa cha Afrika ACDC profesa John Nkengasong amesema, kuna uwezekano wa kuwepo kwa maambukizi yasiyoripotiwa, lakini nchi za Afrika zimejiandaa vizuri, kama kuna wagonjwa, zitagundua na kuripoti mara moja.

    Profesa wa Taasisi ya Utafiti wa Afya na Udaktari wa Sehemu za Joto ya Uingereza Jimmy Whitworth amesema, uchache wa maambukizi ya COVID-19 barani Afrika labda unatokana na hatua madhubuti zilizochukuliwa na nchi za bara hilo. Mwishoni mwa mwezi Januari, nchi zilizoweza kupima virusi vya ugonjwa huo barani Afrika zilikuwa Afrika Kusini na Senegal tu, lakini sasa nchi zaidi ya 40 zimepata uwezo huo.

    Profesa Nkengasong amesema, Afrika inakabiliwa na changamoto mbili katika kukabiliana na COVID-19, ya kwanza ni uwezo wa kugundua na kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo kwa haraka, na ya pili ni matishio ya magonjwa mengine ya kuambukiza ikiwemo Malaria na Surua, ambayo yanachukua rasilimali ya matibabu.

    Hata hivyo, Afrika pia ina uwezo maalumu wa kukinga COVID-19. Ikilinganishwa na nchi za Ulaya na nchi nyingine zilizoendelea, nchi za Afrika zina vijana wengi zaidi, na takwimu zilizotolewa na WHO zinaonesha kuwa ugonjwa huo ni hatari zaidi kwa wazee kuliko vijana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako