• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Trump atangaza dharura ya kitaifa na kuruhusu serikali kutoa msaada wa kupamba na virusi

    (GMT+08:00) 2020-03-14 18:53:03

    Rais wa Marekani Donald Trump jana alitangaza dharura ya kitaifa ambapo ataruhusu Shirika la Serikali la Usimamizi wa Dharura kutoa msaada wa dola za kimarekani bilioni 50 ili kusaidia kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona COVID-19 katika nchi nzima.

    Rais Trump amesema anampa uwezo waziri wa afya na huduma za binadamu kusamehe baadhi ya sheria na taratibu ili kuhakikisha virusi vinadhibitiwa na wagonjwa wanatibiwa. Pia amesema ameamuru kila jimbo nchini kuweka vituo vya dharura kwa lengo la kusaidia kuzuia kuenea kwa ugonjwa.

    Tangazo hilo la dharura ya kitaifa litafungua rasilimali za ziada na mamlaka kwa majimbo kama Washington ambayo yako mstari wa mbele katika kupambana na janga hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako