• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yasema Ulaya sasa yawa kitovu cha mlipuko wa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-14 18:53:46

    Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema Ulaya sasa imekuwa kitovu cha mlipuko wa COVID-19, huku zikiripotiwa kesi na vifo vingi zaidi kuliko maeneo mengine duniani, mbali na China.

    Amesema kesi nyingi sasa zinaripotiwa kila siku kuliko zilizoripotiwa China wakati hali ya mlipuko ilipokuwa mbaya. Amesisitiza kuwa ni janga la kutisha ambapo watu 5,000 wamefariki kwa COVID-19 duniani, huku zaidi ya kesi 132,000 zikiripotiwa kwa WHO kutoka nchi na maeneo 123.

    Amezitaka nchi zote kuchukua tahadhari ya kina, akisisitiza kuwa virusi vinaweza kumpata yeyote. Amebainisha kuwa kutokana na uzoefu kutoka nchi kama China, hatua kali za kupima na kutafuta watu waliowasiliana na mtu mwenye virusi, pamoja na kutenga watu kwenye jamii na uhamasishaji wa jamii, zinaweza kuzuia maambukizi na kuokoa maisha.

    Habari nyingine zinasema, rais Xi Jinping wa China amesema, China iko tayari kutoa msaada kwa Ulaya katika kupambana na COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako