• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atoa salamu kwa viongozi wa Korea Kusini, Iran, Italia na Umoja wa Ulaya kuhusu maambukizi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-14 19:01:17

    Rais Xi Jinping wa China leo ametoa salamu za dhati kwa viongozi wa Korea Kusini, Iran, Italia na Umoja wa Ulaya zinazokumbwa na hali mbaya ya maambukizi ya COVID-19 pamoja na serikali na watu wa nchi hizo tatu kwa niaba ya serikali ya China na watu wake.

    Kwenye salamu zake Rais Xi amesisitiza kwa rais Moon Jae-in wa Korea Kusini kuwa, China inapenda kushirikiana na Korea Kusini na kuyashinda maambukizi ya COVID-19 mapema iwezekanavyo, na kulinda usalama wa maisha na afya za watu wa nchi hizo mbili na watu wa dunia nzima.

    Ka upande wa salamu alizozitoa kwa rais Hassan Rouhani wa Iran, rais Xi amesema, China na Iran ni marafiki wa kimkakati wa pande zote, na China inataka kuimarisha ushirikiano na Iran katika kupambana na maambukizi ya COVID-19 na kuendelea kutoa msaada kwa Iran kadiri iwezekanavyo.

    Aidha wakati anatoa salamu zake kwa rais Sergio Mattarella wa Italia, rais Xi amesema China, Italia na Jumuiya ya kimataifa zikishirikiana kufanya juhudi, zitashinda matatizo kwa pamoja na kuyashinda maambukizi ya COVID-19 mapema iwezekanavyo, na kulinda afya na utulivu wa watu wa nchi mbili na watu wa duniani.

    Alipotoa salamu kwa Umoja wa Ulaya, rais Xi amasema China iko tayari kutoa msaada wa umoja huo katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako