• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya kimataifa yaisifu China kuchagia uzoefu wa kupambana na maambukizi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-15 19:26:32

    Wakati maambukizi ya COVID-19 yanasambaa kwenye sehemu mbalimbali duniani, China imefanya juhudi kudhibiti maambukizi hayo nchini humo na pia imeanzisha ushirikiano wa kimataifa na nchi mbalimbali duniani kuhusu kudhibiti na kukinga maambukizi hayo, na kusifiwa sana na jumuiya ya kimataifa.

    Waziri wa mambo ya nje wa Italia Bw. Luigi Di Maio amesema wataalamu wa China wameleta msaada ambao utawaokoa wagonjwa wa Italia.

    Msemaji wa wizara ya afya ya Iran Bw. Kianoush Jahanpur amesema ujumbe wa wataalamu wenye uzoefu wa kupambana na COVID-19 wa China unashirikiana na wataalamu wa Iran, na Iran inahitaji kujifunza kutoka mafanikio ya China ili kufuata njia iliyo sahihi.

    Rais Azali Assoumani wa Comoro amesema China inabadilishana uzoefu wake na nchi mbalimbali duniani, kitendo hicho kinaonesha uwajibikaji wa China. Rais Mokgweets Masisi wa Botswana ameisifu China kwa kuchukua hatua madhubuti kudhibiti na kutibu ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako