• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la Uhamiaji la Kimataifa IOM laomba uungaji mkono wa dola za kimarekani milioni 77.6 kwa ajili wa watu milioni 1.2 Ethiopia

    (GMT+08:00) 2020-03-15 19:31:45

    Shirika la Uhamiaji la Kimataifa IOM limezindua mpango wa kuomba uungaji mkono wa dola za kimarekani milioni 77.6 ili kutoa msaada wa kibinadamu kwa wakimbizi wa ndani, wahamiaji na watu wanaorudi nyumbani wapatao milioni 1.2, pamoja na jamii zinazowahifadhi.

    Taarifa iliyotolewa jana na shirika hilo inaitaka jumuiya ya wahisani kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa watu hao wa Ethiopia kwa mwaka huu na baadaye.

    IOM imesema Ethiopia imeendelea kupokea wahamiaji na wakimbizi, na kuanzia mwezi Januari hadi mwezi Oktoba imepokea jumla ya wakimbizi na wahamiaji 88,044 kutoka nchi jirani hasa Eritrea, Sudan Kusini na Somalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako