• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taasisi ya kupambana na Rushwa Tanzania yaokoa dola milioni 3.8 zilizoibwa kutoka kwa vyama vya ushirika

    (GMT+08:00) 2020-03-15 19:32:10

    Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Tanzania imesema imeokoa shilingi bilioni 8.8 za Tanzania, zilizoibwa vyama vya masoko ya mazao ya kilimo Tanzania AMCOS.

    Kaimu Mkurugenzi wa taasisi hiyo Bw. John Mungo amewaambia wanahabari mjini Dar es salaam, kuwa fedha hizo zimeokolewa kati ya Novemba 2019 na Februari 2020.

    Amesema fedha hizo ni sehemu ya shilingi bilioni 124 ambalo waziri wa kilimo wa Tanzania Bw. Japhet Haonga ameigaiza taasisi hiyo kufanya uchunguzi kufuatia ripoti ya matumizi mabaya yaliyofanywa na maofisa wa AMCOS.

    Bw. Mbungo amesema kati ya fedha zilizookolewa, baadhi zilisalimishwa na maofisa kwa hiari na nyingine zilirudishwa baada ya maofisa wa vyama hivyo kuhojiwa na taasisi ya kupambana na rushwa.

    Mwezi Oktoba mwaka jana Rais John Magufuli alisema taasisi ya kupambana na rushwa iliwakamata maofisa 92 wa vyama vya ushirka kutokana na kuwaibia wakulima wa korosho mkoani Mtwara na Lindi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako