• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Tanzania yakandikwa 5-0 na Uganda U-17

    (GMT+08:00) 2020-03-16 08:38:08

    Timu ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17 jioni ya Jumamosi imefungwa mabao 5-0 na wenyeji, Uganda kwenye mchezo wa marudiano kufuzu Fainali za Kombe la Dunia Uwanja wa Lugogo Jijini Kampala hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 6-2 kufuatia kushinda 2-1 kwenye mechi ya kwanza Machi 1 nyumbani, Dar es Salaam. Hata hivyo kwa upande wa Kikosi cha timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 16 kimeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Liberia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Liberia Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Mabao ya Tanzania inayofundishwa na Maalim Saleh 'Romario' yamefungwa na Thabit Thrishan, Hamisi Mohamed na Boniface James. Mechi mbili za awali baina ya timu hizo, Tanzania ilishinda 3-0 Machi 10 kabla ya kufungwa 3-1 Machi 12. Tanzania na Liberia zimelazimika kucheza mara tatu baada ya waalikwa wengine, Malawi kutotokea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako