• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya korona duniani yazidi laki 1.5

    (GMT+08:00) 2020-03-16 08:57:51

    Takwimu zilizotolewa jana na Shirika la afya duniani (WHO) zimeonesha kuwa, idadi ya jumla ya watu walioambukizwa virusi vya korona duniani imeongezeka na kuzidi laki 1.5.

    Hadi kufikia jana idadi ya watu walioambukizwa virusi vya korona duniani ilikuwa imefikia laki 1.52, kati yao watu 5,720 wamefariki, na maambukizi yameripotiwa katika nchi na sehemu 141 kote duniani.

    Takwimu pia zimeonesha kuwa, idadi ya watu walioambukizwa virusi vya korona nje ya China, imefikia 72,469. WHO limezitaka nchi mbalimbali zichukue hatua mara moja, kuimarisha huduma za matibabu na upimaji, ili kupunguza kuenea kwa virusi hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako