• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini yautangaza mlipuko wa virusi vya korona kuwa Janga la taifa

    (GMT+08:00) 2020-03-16 08:59:00

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ameutangaza mlipuko wa virusi vya korona kuwa Janga la taifa, na kusema nchi yake itachukua hatua mbalimbali ikiwemo zuio la utalii ili kupambana na virusi hivyo.

    Akikutana na wanahabari baada ya kuitisha mkutano wa dharura wa Baraza la mawaziri, rais Ramaphosa ametangaza uamuzi huo na kusema utapunguza kadri iwezavyo madhara yanayotokana na mlipuko wa virusi vya korona, na pia kusaidia kuanzisha mfumo wenye ufanisi wa kukabiliana na janga kama hilo.

    Rais Ramaphosa amesema baada ya tathmini hali ya maambukizi ya virusi vya korona nchini Afrika Kusini na katika nchi nyingine, serikali imeamua kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo zuio la utalii, ili kupunguza athari za mlipuko wa virusi hivyo.

    Mpaka sasa Afrika Kusini imethibitisha maambukizi 61 ya watu, idadi ambayo ambayo ni kuwa kuliko nchi nyingine za Afrika Kusini mwa Sahara.

      

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako