• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yaahirisha duru ya pili ya uchaguzi wa wabunge kutokana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-16 09:44:23

    Msemaji wa Baraza la ulinzi wa Katiba la Iran Bw. Abbasali Kadkhodaei amesema duru ya pili ya uchaguzi wa bunge la Iran itaahirishwa na kufanyika tarehe 11 mwezi Septemba.

    Bw. Kadkhodaei amesema kuwa baraza hilo lilikubali ombi la wizara ya mambo ya ndani ya Iran kuahirisha uchaguzi huo uliopangwa kufanyika tarehe 17 Aprili kutokana na kuenea kwa COVID-19.

    Wakati huo huo, idadi ya jumla ya watu walioambukizwa nimonia ya COVID-19 nchini Iran imeongezeka na kukaribia elfu 14, na watu 724 wamefariki kutokana na ugonjwa huo, na zaidi ya 451 wamepona.

    Aidha wizara ya afya wa Iran imehimiza kusitishwa kwa safari za msimu wa mwaka mpya wa Iran unaoanzia tarehe 20 mwezi Machi, ili kuzuia kuenea kwa virusi.

    Rais Hassan Rouhani wa Iran ameamua kufuta uwezekano wa kufunga mji mkuu wa Tehran na miji mingine. Kamanda wa jeshi la Iran Bw. Kiomars Heidari amesema jeshi la Iran lilizindua zoezi la upimaji wa virusi vya korona katika majimbo ya Qom na Gilan ili kukabiliana na mlipuko wa COVID-19, na zoezi hilo litatekelezwa nchini kote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako