• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ezequiel Garay aibuka mchezaji wa kwanza La Liga kugunduliwa na corona

    (GMT+08:00) 2020-03-16 16:07:04

    Ezequiel Garay ni mchezaji wa kwanza wa La Liga kupatwa na virusi vya ugonjwa hatari wa corona. Raia huyo wa Argentina alipimwa pamoja na wachezaji wote wa timu ya kwanza ya Valencia kabla ya klabu hiyo kufuta shughuli zake zote hadi mwishoni mwa Machi. Mchezaji huyo mwenye miaka 33 alikosa mechi zote za Valencia za Ligi ya Mabingwa na kupoteza kwa Atalanta kwa sababu alikuwa majeruhi na kuwa nje msimu huu mzima. Mlinzi huyo kwa sasa amejitokeza kufichua kupitia mtandao jamii kuwa anaugua homa ya corona. Wachezaji kadhaa wamekutwa na maambukizi ya korona ikiwa ni pamoja na Patrick Cutrone anayekipiga kwa mkopo wa Fiorentina na staa wa Chelsea, Callum Hudson-Odoi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako