• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kocha wa Arsenal Mikel Arteta azungumzia afya yake baada ya kupatwa na corona

    (GMT+08:00) 2020-03-16 16:07:23

    Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amewatoa hofu mashabiki na kuwakikishia kuwa anaendelea vyema siku chache baada ya kuthibitishwa kuwa na virusi vya korona. Alhamis iliyopita, Arteta alithibitisha kuwa anaugua ugonjwa huo hatari, huku taarifa rasmi kutoka Arsenal ikisema kuwa atajitenga kulingana na sheria za serikali kuhusu afya. Huku kukiwa na hofu kuhusu hali yake ya afya, Arteta sasa amechukua hatua ya kuwahakikishia wafuasi kuwa anaendelea kupona na kukiri kwamba nyanja ya soka inakumbwa na changamoto kubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako