• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wanaoingia Beijing kutoka nchi za nje kutengwa kwa siku 14 kwa ajili ya uchunguzi wa afya 

    (GMT+08:00) 2020-03-16 17:13:35

    Naibu katibu mkuu wa serikali ya Beijing Bibi Chen Bei jana amesema, kuanzia leo, watu wote wanaoingia mjini Beijing kutoka nchi za nje watapelekwa kwenye kituo cha uchunguzi wa afya na kuwa kwenye karantini kwa siku 14, ili kuzuia kuingia na kuenea kwa virusi vya korona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 mjini humo kutoka nchi za nje.

    Amesema madaktari na wauguzi watafanya uchunguzi wa afya za watu hao, na kuchukua hatua haraka kama wagonjwa wakipatikana. Watu ambao watagundulika kutoa taarifa zisizosahihi au kuficha ugonjwa na kusababisha kuenea kwa virusi, watafikishwa mbele ya sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako