• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Corona yatikisa sekta ya utalii Kenya.

    (GMT+08:00) 2020-03-16 18:42:00
    Wawekezaji katika sekta ya Utalii wameingiwa na wasiwasi baada ya Kenya kuthibitisha kuwepo kwa virusi vya corona nchini. Sekta hiyo imeathiriwa baada ya wageni kukatiza ziara zao kuja Pwani kutokana na maradhi hayo na safari za ndege kusitishwa.

    Ijumaa iliyopita, Waziri wa Utalii Najib Balala alikiri kwamba sekta hiyo imeathiriwa pakubwa.

    Utalii unatarajiwa kudorora zaidi baada ya serikali kuu kusitisha mikutano yote ya kimataifa iliyokuwa inatarajiwa mwezi huu wa Machi. Kwa sasa msimu huo ambao hauna wageni wengi unajikokota baada ya ugonjwa huo kusambaa kwa kasi sana katika mataifa mengi duniani.

    Hoteli ya Pride Inn Paradise, Shanzu, ilikuwa inatarajia kuwa na wageni wa kimataifa kwenye kongamano la 63 la wawekezaji wa viwanja vya ndege, Jumamosi iliyopita, lakini warsha hiyo ilifutiliwa mbali.

    Mkutano huo wa kimataifa ulikuwa uwalete pamoja zaidi ya wageni 400 ambao wengine walitarajia kukodi hoteli jirani ya Serena.

    Aidha wamiliki wa hoteli wanaomba muungano wa benki nchini kuwawia radhi wenye madeni au mikopo wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako