• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Lipia bidhaa na huduma kwa kutumia kadi au kwa njia ya simu.

    (GMT+08:00) 2020-03-16 18:42:23
    Kama njia moja ya kuzuia maambukizi na kuenea kwa kasi kwa virusi vya corona, rais Uhuru Kenyatta amewasihi Wakenya kukumbatia teknolojia katika kulipia huduma na kununua bidhaa madukani.

    Rais anawataka wakenya kujiepusha kutumia pesa taslimu kwani hii inaweza kuchangia kueneza virusi hivi. Wakenya wanaombwa kutumia malipo ya simu au kadi za atm.

    Wakati uo huo, rais Uhuru ameomba kampuni za mawasiliano zenye kutoa huduma za kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu, kupunguza ada wanazotoza wateja wao, ili kuwezesha kila mmoja kutumia njia hii ya kulipia na kununua bidhaa.

    Aidha, rais pia ametoa onyo kali kwa wafanyibiashara ambao huenda wanapanga kuongeza bei ya bidhaa na huduma muhimu wakati huu Kenya inapokabiliana na virusi vya Corona. Rais amesema kwamba mfanyibiashara yeyote atakayepatikana na hatia hii, basi atakamatwa.

    Huku hayo yakijiri, Chama cha Wauza Vileo Nchini Kenya (ABAK) kimetangaza kuwa kiko tayari kusalimu amri endapo serikali itaamuru kwamba vilabu vyote vya usiku vifungwe kutokana na kero la virusi vya corona.

    Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari mwenyekiti wa chama hicho Gordon Mutungi alisema wataunga mkono hatua kama hiyo kwa sababu janga hilo lina madhara makubwa kuliko kampuni au sekta yoyote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako