• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Fursa za uwekezaji zawekwa wazi kwa wawekezaji wa kigeni.

    (GMT+08:00) 2020-03-16 18:43:14
    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, idara ya uwekezaji, Angella Kairuki, ameyaainisha maeneo na sekta mbali mbali zenye fursa nyingi za uwekezaji nchini. Bi Kairuki amewataka wawekezaji kutoka Sweden kuja na kuchangamkia fursa hizo.

    Akizungumza kwenye kongamano la Biashara na uwekezaji la Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Bi Kairuki amabaye alikuwa amemwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aliwahakikishia wawekezaji hao kwamba serikali imeweka mikakati imara ya kuwawezesha kuwekeza Tanzania.

    Hafla hiyo ilihudhuriwa na wafanyibiashara na wawekezaji kutoka Sweden. Sekta ya Utalii ni mojawapo yenye fursa nyingi nchini Tanzania kwa wawekezaji wa kigeni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako