• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafuatilia mlipuko wa COVID-19 nchini Iran

    (GMT+08:00) 2020-03-16 19:47:48

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inafuatilia sana maendeleo ya mlipuko wa ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona (COVID-19) nchini Iran, na inapenda kutoa misaada kwa nchi hiyo kadri iwezavyo.

    China pia imetoa wito jumuiya ya kimataifa kuongeza ushirikiano na Iran katika kupambana na virusi hivyo ili kulinda kwa pamoja usalama wa afya duniani.

    Aidha, Bw. Geng pia amesema, kikosi cha matibabu cha China kilichowasili Roma, wiki iliyopita kimeanza kufanya kazi ya kusaidia Italia kupambana na virusi moja kwa moja. Amesema kikosi hicho kimesifiwa na kupongezwa na Italia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako