• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Virgil van Dijk asema itasikitisha endapo watatwaa ubingwa wa Ligi Kuu England bila mashabiki

    (GMT+08:00) 2020-03-17 08:22:46

    Beki wa Liverpool Virgil van Dijk amesema ni jambo kusikitisha endapo watatwaa ubingwa wa Ligi Kuu England bila mashabiki wao. Liverpool ina nafasi ya kumaliza ukame wa kutotwaa ubingwa wa mashindano hayo baada ya miaka 30. Timu hiyo inahitaji kushinda angalau mechi mbili kutangazwa mabingwa wapya. Wakati Ligi Kuu England imesitishwa hadi Aprili 3 kutokana na maambukizi ya virusi vya korona, Liverpool iko mbele kwa pointi 25. Hata hivyo, libero huyo alisema uamuzi huo hauwezi kuwaweka kando katika mstari wa kutwaa ubingwa msimu huu. Hadi sasa hakuna uamuzi rasmi uliotolewa na Chama cha Soka England (FA) kuhusu mustakabali wa mashindano hayo kama yatafutwa au vinginevyo msimu huu. Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anatarajiwa kutoa tamko kuhusu matukio yenye mikusanyiko ikiwemo michezo kutokana na janga hilo la korona. Vigogo wa Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) watazungumza leo kuhusu upangaji wa ratiba ya Fainali za Ulaya zilizopangwa kuanza Juni 12.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako