• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Yanga SC yafanunua kwanini pesa walizoahidiwa wachezaji wake zimechelea kutolewa

    (GMT+08:00) 2020-03-17 08:23:52

    Afisa muhamasishaji mkuu wa Yanga SC Antonio Nugaz jana alitolea ufafanuzi madai ya baadhi ya mashabiki mtandaoni kuwa wachezaji wa Yanga SC wamecheza chini ya kiwango katika mechi dhidi ya KCM waliyofungwa 1-0 na mechi dhidi ya Namungo waliyotoka sare ya 1-1 kutokana na kutopewa bonas yao ya Tsh milioni 200. Yanga kuelekea mechi ya Simba walioyoshinda 1-0 waliahidiwa na mdhamini wao GSM kwa mujibu wa vyombo vya habari bonus ya Tsh milioni 200 kama wataifunga Simba SC, hivyo baada ya kucheza chini ya kiwango kwa game mbili mfululizo zilizofuatia baada ya ushindi dhidi ya Simba SC, wengi wakadai ni kutokana na kutotimiziwa ahadi yao. Nigaz amesema ni kweli malipo yamechelewa na sababu kubwa ni kutokana na taratibu za kibenki, kwani Tsh milioni 200 ni tofauti na Tsh milioni 10 ambayo kwa kawaida hutolewa kila mechi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako