• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia yaahidi kuongeza juhudi za kupambana na COVID-19 baada ya kuthibitisha kisa cha kwanza

    (GMT+08:00) 2020-03-17 09:28:36

    Serikali ya Somalia imeahidi kuongeza juhudi za kupambana na COVID-19 baada ya kuthibitisha mtu wa kwanza mwenye virusi hivyo mjini Mogadishu.

    Waziri wa afya wa Somalia Bibi Fawziya Abikar Nur amewataka wasomali wawe macho na kuchukua hatua za kinga kwa makini. Bibi Abikar amesema, mtu aliyeambukizwa ni raia wa Somalia ambaye ni miongoni mwa watu wanne waliowekwa kwenye karantini baada ya kurudi Somalia kutoka nchi iliyokumbwa na COVID-19 wiki iliyopita.

    Amesema wizara ya afya ya Somalia ilipata matokeo ya upimaji kutoka nchi ya nje, vilevile wizara hiyo itafanya juhudi zote kuilinda nchi hiyo dhidi ya virusi hivyo. Wakati huo huo, wizara ya uchukuzi na usafiri wa anga ya Somalia imetangaza kupiga marufuku kwa wiki mbili safari za ndege za kimataifa kuanzia Jumatano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako