• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya maambukizi ya COVID-19 nchini Italia yazidi elfu 23

    (GMT+08:00) 2020-03-17 10:10:05

    Mkuu wa idara ya ulinzi wa raia ya Italia Bw. Angelo Borrelli amesema watu 2,500 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Korona nchini Italia katika saa 24 zilizopita, na kufanya idadi ya jumla ya idadi ya watu walioambukizwa kuwa zaidi ya elfu 23, lakini ongezeko hilo linaweza kuashiria kilele cha mlipuko wa ugonjwa huo nchini Italia, kwani kiwango cha ongezeko ni cha chini zaidi kwa asilimia tangu tarehe 1 mwezi Machi.

    Bw. Borrelli anatumai kuwa Italia itaendelea kushuhudia kupungua kwa kiwango cha ongezeko, hivyo wanaweza kuwa na uhakika zaidi kuwa nchi hiyo imechukua hatua madhubuti.

    Mwenyekiti wa Kamati kuu ya afya ya Italia Bw. Franco Locatelli amesema itabidi kusubiri kwa siku chache zaidi kuona kupungua kwa idadi ya maambukizi, lakini la muhimu zaidi ni kupungua kwa idadi ya wagonjwa mahututi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako