• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: City Stars yazidi kutetemesha kipute

    (GMT+08:00) 2020-03-17 16:09:12

    Timu ya Nairobi City Stars iliendelea kutetemesha wapinzani wao kwenye kampeni za kufukuzia taji la Betika Supa Ligi ya Taifa Kenya (BNSL) baada ya kuifunga Nairobi Stima bao 1-0 kwenye mechi iliyopigiwa Uwanjani Camp Toyoyo Jericho, Nairobi. City Stars maarufu Simba wa Nairobi ilionyesha mechi safi na kuhakikisha inabeba pointi tatu muhimu ili kuendelea kujiongezea matumaini ya kutwaa ubingwa wa taji hilo na kufuzu kushiriki Ligi Kuu ya KPL msimu ujao. City Stars ilipata bao hilo la pekee kupitia juhudi zake, Ebrima Sanneh. Kwenye matokeo ya mechi nyingine kuwania taji hilo, Administration Police (AP) iliona giza ugenini iliponyukwa mabao 3-1 na wenyeji wao Coast Stima katika patashika iliyopigiwa Uwanjani Mbaraki Sports, mjini Mombasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako