• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jack Ma kutoa mask na vifaa vya kupima virusi vya corona kwa nchi zote 54 za Afrika

    (GMT+08:00) 2020-03-17 16:49:58

    Bilionea wa China na mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Alibaba Jack Ma amesema atatoa mask, mavazi ya kujikinga na vifaa vya kupima virusi vya corona kwa nchi zote barani Afrika.

    Mfuko wa Ma umesema mask milioni 6, vifaa vya kupima virusi milioni 1.1, nguo za kujikinga elfu 60 na kofia zinazofunika uso elfu 60 zitapelekwa kwa pamoja mjini Addis Ababa, na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed atasaidia kuzisambaza kwa kila nchi barani Afrika.

    Vilevile, amesema Mfuko huo utashirikiana na taasisi za matibabu za nchi mbalimbali za bara hilo ili kutoa mafunzo kupitia mtandao wa internet kuhusu matibabu kwa wagonjwa wenye maambukizi ya virusi vya corona.

    Msaada huo kwa nchi za Afrika ni wa hivi karibuni kufanywa na Mfuko wa Jack Ma na Kampuni ya Alibaba kuunga mkono juhudi za dunia katika kupambana na mlipuko huo. Tayari kampuni hiyo imepeleka misaada ya kupambana na virusi vya korona katika nchi za Japan, Korea Kusini, Marekani, Italia na Hispania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako