• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa walaani shambulizi dhidi ya walinda Amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

    (GMT+08:00) 2020-03-17 17:07:55

    Umoja wa Mataifa umelaani vikali shambulizi lililofanywa na wapiganaji wenye silaha dhidi ya Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja huo nchini Afrika ya Kati lililosababisha kifo cha askari mmoja wa kulinda amani.

    Jumapili iliyopita, wapiganaji hao waasi wanaofahamika kama anti-Balaka, chini ya uongozi wa Dimitri Ayoloma, walifanya shambulizi katika mji wa Grimari, na kumuua askati mmoja wa kulinda Amani raia wa Burundi aliyejaribu kuzuia shambulizi hilo.

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema, shambulizi dhidi ya walinda amani ni sawa na uhalifu wa kivita chini ya sheria ya kimataifa, na kuitaka serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kufanya kila linalowezekana kuwafikisha washambuliaji hao mbele ya sheria.

    Nchi wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zimetoa salamu za rambirambi kwa familia ya askari huyo, na kulaani vikali mashambulizi yote, na uhalifu dhidi ya kikosi cha kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako