• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya Ada za Mpesa zapunguzwa

    (GMT+08:00) 2020-03-17 19:17:33
    WAKENYA wanaotuma Sh1,000 kwenda chini kwa njia ya simu hawatatozwa ada yoyote kwa miezi mitatu ijayo kuanzia leo, baada ya kampuni za Safaricom, Airtel na Telcom kuondoa ada hizo.

    Hatua hiyo iliafikiwa Jumatatu baada ya mkutano kati ya maafisa wakuu wa kampuni hizo na Gavana wa Benki Kuu ya Kenya Dkt Patrick Njoroge.

    Hatua hiyo pia inafuatia ombi la Rais Kenyatta kwa kampuni zinazotoa huduma za utumaji pesa kwa njia ya simu, kutafuta njia mbadala za kuwapunguzia Wakenya hatari ya kuambukizwa virusi vya corona wanapolipia bidhaa kwa pesa taslimu.

    Kwenye taarifa, kampuni ya Safaricom pia iliongeza kiwango ambacho mtu anaweza kutuma ama kutoa kwa njia ya M-Pesa kutoka Sh70,000 kwa siku hadi Sh150,000.

    Wakenya vile vile wataweza kuweka hadi Sh300,000 kwa simu kutoka Sh140,000 kwa sasa.

    Hatua hii pia inalenga kuwasaidia wenye biashara ndogo ndogo, amesema Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni hiyo Michael Joseph.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako