• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi waathirika kufuatia visa vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-03-17 19:18:09
    Kusitizwa kwa shughuli na watu kuambiwa wakae nyumbani Kenya imeanza kutembea chini ya njia ya mataifa ambayo uchumi wao umeharibiwa na Covid-19.

    Kampuni zinajaribu kujua wapi kupata pesa za kuwalipa wafanyikazi wao mwishoni mwa mwezi kwa sababu ya athari za kushuka kwa uchumi kwa sababu ya juhudi za kupigana na virusi.

    Kampuni zingine zimeamua kujihusisha na watu wa kawaida wakati wanaamua jinsi ya kulipa wafanyikazi wa kudumu.

    Muungano wa Sekta ya Kibinafsi ya Kenya (Kepsa) imesema itaendeleza jukwaa la hatua ya biashara ya Covid-19 katika siku mbili zijazo, kama nchi zingine zilivyofanya.

    Mtendaji Mkuu wa Kepsa Carole Karuga amesema Jukwaa hilo litakuwa na kituo cha kupiga simu cha masaa 24 na kituo ya kutoa habari za biashara zinazohusiana na mahali pa kazi kwa sekta zote ikiwa ni biashara kubwa, biashara ndogo na za kati (SMEs) hadi kwa kimataifa, na mfumo juu ya athari ya uchumi ya virusi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako