• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa na wataalamu wa China na Afrika kufanya mkutano wa video kuhusu COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-03-17 19:34:18

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang amesema, maofisa na wataalamu wa China na Afrika watafanya mkutano kwa njia ya video, ili kubadilishana habari na uzoefu kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa nimonia inayosababishwa na virusi vipya vya korona (COVID-19).

    Geng amesema China na nchi za Afrika ni marafiki wakubwa, na katika muda mrefu uliopita, zimesaidiana na kushirikiana vizuri, tangu kutokea kwa maambukizi ya ugonjwa huo nchini China, nchi za Afrika zimeiunga mkono na kutoa msaada halisi kwa China.

    Geng amesema hivi sasa juhudi za kukabiliana na COVID-19 nchini China zina mwelekeo mzuri, wakati China inaendelea kupambana na maambukizi ya ndani ya ugonjwa huo, itatoa msaada kwa Afrika kadiri inavyoweza, na hadi sasa imetoa vifaa vya kupima virusi vya korona na misaada mingine kwa nchi za Afrika zilizoathiriwa na ugonjwa huo.

    Aidha, Geng amesema China itashirikiana na Afrika ili kutekeleza viruzi ushirikiano wao katika sekta ya afya chini ya Baraza la Ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako