• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Pakistan wafanya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2020-03-17 20:17:57

    Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na mwenzake wa Pakistan Arif-ur-Rehman Alvi ambaye yupo ziarani nchini China.

    Rais Xi amesisitiza kuwa, hivi sasa virusi vya korona (COVID-19) vimeenea katika nchi nyingi duniani, na nchi zote zinapaswa kushirikiana kukabiliana na ugonjwa huo. Amesema China itaendelea kutoa msaada kwa Pakistan katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

    Rais Xi amesema bila kujali mabadiliko ya hali ya dunia, China siku zote iko pamoja na Pakistan, na itaendelea kuiunga mkono nchi hiyo kulinda uhuru wa kitaifa na ukamilifu wa mamlaka na ardhi, na kuiunga mkono kupata njia ya kujiendeleza inayolingana na hali halisi ya nchi hiyo.

    Kwa upande wake, Rais Alvi amesema, wakati wa janga la ugonjwa, Chama cha Kikomunisti cha China na serikali ya China zimeonesha uwezo mkubwa wa kuongoza na kuhamasisha watu, na China imekuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa nchi nyingine katika kukabiliana na COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako