• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KORONA: CAF yaahirishwa fainali CHAN huku TFF ikisimamisha ligi zake zote

    (GMT+08:00) 2020-03-18 08:23:42

    Shirikisho la soka Afrika CAF limetangaza kuahirishwa kwa fainali za michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN). CAF imetangaza kuahirisha fainali hizo ikiwa zimesalia siku chache kabla ya kuanza April 4 na kumalizika April 25 nchini Cameroon, wameahirisha hivyo kutokana na kuenea kwa virusi vya corona. Hata hivyo kabla ya taarifa hizo kutoka, timu ya taifa ya Morocco na Rwanda zilitangaza kujitoa kwa hofu ya virusi vya korona. Nalo shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesimamisha ligi zake zote ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufuatia mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa COVID 19 ambao umeingia nchini humo. Pia TFF imevunja kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars ambayo ilikuwa inajiandaa na fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) zilizopangwa kuanza Aprili 4 hadi 25, mwaka huu nchini Cameroon. Taarifa ya TFF imesema kwamba kikao cha Kamati ya Uongozi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kilichoitishwa na Rais wa shirikisho hilo, Wallace Karia kitafanyika kama kawaida leo Saa 3:00 asubuhi hoteli ya Golden Tulip Jijini Dar es Salaam, lakini kwa lengo la kutoa mwelekeo wa utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako