• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KORONA: Mason Mount amuomba msamaha Kocha Frank Lampard kwa kukaidi kujikinga na korona

    (GMT+08:00) 2020-03-18 08:24:11

    Nyota wa timu ya Chelsea Mason Mount amemuomba msamaha Kocha Mkuu wa timu hiyo Frank Lampard kwa kosa lake la kuonekana akicheza mpira akiwa na Declan Rice licha ya kukatazwa kufanywa hivyo kwenye mjumuiko wa watu. Katazo hilo lilikuja baada ya uongozi wa Chelsea kuwaambia wachezaji wake kutochangamana na watu kutokana na agizo la Serikali kuwataka waliokaribu na wagonjwa kujitenga kwa muda wa siku 14 na jamii kwani mchezaji wao Callum Hudson-Odoi aligundulika na Virusi vya Korona wiki iliyopita. Kiungo huyo alionekana akifurahia mtaani na rafiki yake Declan Rice kwenye kituo cha Trent Park siku ya Jumapili. Kikosi cha kwanza cha Chelsea kilipata nafasi ya kuwa na mawasiliano ya karibu na nyota Hudson-Odoi walipokuwa kwenye kambi na ametakiwa kutoonana na wenzake kwa muda wa siku 14 baada ya kungundulika na Virusi vya Korona. Kitendo hicho kilimfanya Kocha wa Chelsea, Frank Lampard kuzungumza na Mount kwa njia ya simu na mchezaji huyo aliomba msamaha kwa kushindwa kutimiza masharti kwani alikuwa anatambua kwamba hana maambukizi ya Korona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako